Ulishawahi kufikiria Bus linaweza kutumia kinyesi cha Binadamu kutembea?stori iko hapa
Unaweza usiamini ama kufikiria kuwa kinyesi cha binadamu kina thamani kiasi cha kutumika kama mbadala wa mafuta katika gari lakini unaambiwa Basi la kwanza Uingereza linalotumia nishati hiyo limeingia barabarani.
Basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria40 ‘Bio bus’ linatumia gesi itokanayo na kinyesi cha binadamu na takataka nyingine zinazozalishwa kwenye kiwanda kilichopo kusini Magharibi mwa nchi hiyo kuweza kutembea.
Katika Gazeti la UHURU limeandika kuwa tanki moja la gesi hiyo lililozalishwa kutokana na kinyesi cha watu inatosha kuendesha gari hilo kwa umbali wa kilomita305.
Basi hilo rafiki wa mazingira ambalo watengenezaji wake wanasema litaboresha hewa, linaendeshwa kwa nishati ambayo ni ya kawaida,kinyesi cha binadamu ambacho ni miongoni mwa majitaka mengine.
Watengenezaji hao walisema gari hilo la aina yake litaboresha hali ya hewa na kuthibitisha kumbe kuna thamani katika kinye si cha binadamu.
Zipo taarifa kuwa siku si nyingi kinyesi cha binadamu kitaanza pia kuzalisha nishati kwa ajili ya simu za mkononi baada ya wataalam kutoka chuo kikuu cha East Anglia cha nchini humo.
Gesi hiyo inazalishwa katika mtambo wa majitaka wa Wessex Water,unaendeshwa na kampuni ya nishati ya Geneco na ugunduzi ,huo unaweza kuzalisha nishati kwa ajili ya teknolojia inayobebeka kama vile simu za mkononi na hata kompyuta mpakato.
Watetezi wa nishati hiyo wanasema basi hilo ambalo linatarajia kusafirisha abiria 10,000 kwa mwezi,linaonyesha thamani ya takataka na linaonyesha mustakabali mwema katika sekta ya usafiri wa umma.
No comments:
Post a Comment