Baada ya Mabasi ya Mwendokasi, Kivuko cha Mv. Dar, hii ni nyingine kuhusu usafiri Dar
Baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “…
Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs
hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya
South Korea imekubali kutufadhili kujenga flyover nyingine pale.. na
barabara yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita 7.2 na barabara
itaanzia Coco Beach, itapita baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital
na kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli Hassan Mwinyi…”
“..
Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna mradi wa BRT ambao una-involve
kilometa zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi unaisha chini ya
ufadhili wa Benki ya Dunia, lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na
tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic count ya magari yanayopita
pale kwa siku yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja elfu kwa hiyo
hawawezi wakaya-accommodate magari yote yanayoweza kupita sehemu hiyo…”– Dk. Magufuli
No comments:
Post a Comment