MABAKI YA MH 17 KUREJESHWA UHOLANZI
Mabaki ya ndege ya MH 17
Shirika
la ulinzi la ulaya,limearifu kwamba mabaki ya ndege ya shirika la ndege
la Malaysia yaliyookotwa huko mashariki mwa Ukraine hatimaye
yanarejeshwa Uholanzi.
Mkuu wa
shirika hilo Michael Bociurkiw ameiambia BBC mabaki yaliyokusanywa na
timu ya uchunguzi kutoka Ujerumani, ambao wamekwisha ingia katika ardhi
inayo dhibitiwa na serikali ya Ukraine na mabaki hayo yatasafirishwa kwa
ndege kutoka katika mji wa Kharkiv.BBC
Timu hiyo
ya watafiti wa Kijerumani inaongoza timu ya watafiti wa kimataifa
kufuatia ajali hiyo ya ndege iliyotokea mwezi July kutokana na maombi
maalumu ya serikali ya Ukraine.
Ndege hiyo iliondoka katika uwanja wa Amsterdam na idadi kubwa kati ya abiria 298 ya waathirika wa tukio hilo ni Wajerumani .
Juhudi za
uchunguzi huo zinakwamishwa na mgogoro unaoendelea huko Mashariki mwa
Ukraine kati ya Urusi na nchi hiyo mgogoro ambao unaungwa mkono na
askari wa majeshi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment