Makala ya
 Ndoto ya Afrika inaeleza habari kuhusu Wajasiriamali wanane kutoka 
maeneo mbalimbali ya Afrika kila mmoja akieleza changamoto alizozipata 
alipokua akianza.Hivyo, katika mfululizo huu utapata fursa ya kujifunza 
katika kufikia ndoto, ndoto zao, na kama waliweza kuzisimamia.CHANZO:BBC
 
            
Mjasiriamali
 Deegbe,hutoa elimu kwa wengine ili kutimiza malengo yaoMbali na kutokua
 na elimu katika soko la viatu, Fred Deegbe, ambaye alikua mfanyakazi wa
 Benki,aliamua kubadili mwelekeo, aliungana na rafiki yake na kuanzisha 
kampuni yao iitwayo, Heel The World (HTW) Kampuni kubwa ya kutengeneza 
viatu yenye makazi yake, Accra Ghana, hiyo ilikua mwaka 2011, na mwaka 
mmoja baadae Deegbe aliacha kazi ya Benki na kuweka nguvu zake katika 
kazi yake hii mpya.
Mjasiriamali huyu mdogo anataka kututhibitishia kuwa viatu vyenye ubora vinaweza kutengenezwa nchini mwake.
Heel The 
World, ambayo ina waajiriwa saba wa kudumu, ina mtandao wake maalum kwa 
ajili ya shughuli zote za kutangaza soko na biashara yake hii inategemea
 mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa, katika shughuli za kutafuta 
masoko.
Ni jinsi gani unaweza kukuza biashara yako kushindana na Soko la bidhaa kutoka China?
Deegbe 
anasema: Bidhaa za China siku zote hazinitii hofu, na sababu kubwa, 
nimejiwekea kanuni mimi na ninaofanya nao kazi, niliweka kanuni hizo 
tangu mwanzo kuwa:
-Ushindani
 ni mzuri wakati wote lakini ni rahisi kumudu, hivyo ninahakikisha 
Kampuni yangu mara zote inatengeneza bidhaa nzuri ili ziweze kupendwa 
kwa namna tunavyotaka.
-Moja ya mikakati niliyonayo tangu awali ni kulenga soko linalofaa.
bidhaa kutoka Heel The World-Nimetumia muda wangu na kuwekeza sana kwenye aina ya bidhaa na soko la bidhaa zangu.
-Tangu mwanzo wa Biashara yangu niliweka akilini kuwa bidhaa ya Kampuni yangu itakuwa ya kutengeneza kwa mkono kuliko mashine.
-Kuwafanya wateja kuwa marafiki. Hili ni suala muhimu sana, kupitia biashara hii, nasaidia pia viwanda vya hapa nyumbani.
Kwa 
sababu Watu hasa vijana wachache wana ajira na kuwa wanakosa elimu ya 
ujasiriamali tuna kitengo cha uwezeshaji kinachowasaidia Watu 
wanaotamani kuwa Wajasiriamali na wengine wanaotaka kuwa wajasiriamali 
wabunifu.
Tumeanzisha Semina tukishirikisha shule za sekondari, Vyuo vikuu pia Taasisi mbalimbali kama UT Bank.
Deegbe 
anasema bidhaa yake inakidhi viwango vya kimataifatunaajiri na 
kushirikiana na Watu wabunifu ambao tunaamini kuwa wanaweza kushidana 
kwenye Soko la Dunia.
Tumekua 
tukitoa mafunzo kwa Watu wanaotaka kujifunza kuhusu utengenezaji wa 
Viatu na kazi nyingine za ngozi, na kuwafundisha namna ya kupata wateja 
kwa mitindo ya aina mbalimbali ya bidhaa.
Kampeni 
ya kuwa washindi katika bidhaa zilizotengenezwa Ghana, 
Afrika:tunathamini bidhaa zetu wenyewe na tumekuwa tukizifanyia kampeni 
kwa miaka mingi kuwa hizi ni bidhaa za nyumbani.
Shanga 
zetu zimetengenezwa kwa vipande vya chupa na shaba nyeupe, vyupa hivyo 
vinatoka kwenye chupa xa Guinness ambazo hutupwa, na shaba kutoka kweye 
vyuma kutoka kwenye magari mabovu ya zamani.
Kulenga 
Soko:tunalenga Soko la bidhaa zetu kupitia mitandao ya kijamii pia kwa 
kuonana ana kwa ana na Wateja, ni biashara ambayo imekua kwa haraka na 
kwa mara zote tumetaka kuwapa Wateja wetu huduma bora na bidhaa zenye 
ubora wa hali ya juu.
Baada ya 
kulifikia Soko la nyumbani na kufanikiwa kwenye hilo, sasa tunadhamiria 
kupeleka bidhaa kwenye Soko la nje, na nimefanikiwa.Hatua hii inahitaji 
Ubora wa hali ya juu.