TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, November 6, 2013

WENGER AWAAMBIA ARSENAL WASUBIRI KUHUSU KUONGEZA MKATABA

wenger 13af2
KOCHA Arsene Wenger atawataka Arsenal wawe na subira juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo hadi watakapofuzu kwa hatua ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. (HM)

Pamoja na hayo, Arsenal wanajiamini kwamba Wenger atasaini Mkataba a kuendelea kufanya kazi ambao utamuwezesha kupata Pauni Milioni 7.5 kwa mwaka Mfaransa huyo.
Wenger, ambaye ametimiza miaka 64 mwezi uliopita, hakutaka Mkataba wake ujadiliwe katika kipindi hiki cha ratiba ngumu kwa timu.
Arsenal inakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Borussia Dortmund kesho Jumatano kabla ya kusafiri hadi Manchester kwa ajili ya kumenyana na mabingwa watetezi, United Uwanja wa Trafford Jumapili.
Wapo katika kundi gumu kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na Marseille na Napoli na Wenger anatarajiwa kusubiri hadi baada ya hapo ndipo ataamua kuhusu mustakabali wake. (HM)

No comments:

Post a Comment