Taarifa kuhusu Watuhumiwa waliomvamia Dr. Sengondo Mvungi

Watuhumiwa
 tisa wanaotajwa kuhusika katika tukio la kuvamia, kuiba na kumjeruhi 
mjumbe wa tume ya kukusanya na kuratibu maoni ya katiba mpya Dr. 
Sengondo Mvungi, wanashikiliwa na jesi la polisi Dar es salaam wakiwa na
 kidhibiti cha mapanga matano yaliyotumika kutekekeleza uhalifu huo.
Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi amesema pamoja na 
mapanga, watuhumiwa hao wamekutwa na simu moja iliyoibiwa siku ya tukio 
pamoja na kigoda ambacho kilitumika kufanikisha hilo zoezi.
Alietajwa kuhusika zaidi kwa kupanga tukio lenyewe ni fundi ujenzi 
Msigwa Mopela aliejenga nyumba ya Dr. Mvugi ambapo Chibago Magosi nae 
alishirikiana na fundi huyu.
Waziri Nchimbi anasema kuhusu kutokamilika kwa upelelezi wa matukio 
mengine ya kujeruhi na kutekwa likiwemo la Dr. Steven Ulimboka pamoja na
 tukio la kuvamiwa kwa Mhariri mtendaji wa gazeti la Mtanzania Absaloom 
Kibanda, Dr. Nchimbi amesema matukio yanatofautiana.
Kukamatwa kwa Watuhumiwa hawa kumetokea siku nane baada ya kujeruhiwa
 kwa Dr. Mvungi aliyeko nchini South Africa kwa ajili ya matibabu.
No comments:
Post a Comment