TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 12, 2013

WENGER ATAKA KUMTIA PINGU YA MIAKA MINNE MERTESACKER 

arsernal 887f4
KLABU ya Arsenal inajiamini beki wake tegemeo, Per Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa muda mrefu. (HM)

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani juu ya vipengele vya Mkataba na inafahamika mazungumzo yanaendelea vizuri.
Mertesacker amedhihirisha yeye ni mwamba wa safu ya ulinzi ya The Gunners akitengeneza ukuta mgumu wa mabeki wanne akicheza sambamba na Laurent Koscielny.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza miezi 18 katika Mkataba wake wa sasa, ambao unamfanya alipwe mshahara wa Pauni 65,000 kwa wiki na kocha Arsene Wenger anataka mustakabali wake ukamilishwe haraka iwezekanavyo.
Na ikiwa mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa, Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa miaka minne, ambao utahusisha kupanda kwa maslahi yake kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Baada ya kuwa mwanzo na mgumu Uwanja wa Emirates, hatimaye beki huyo wa nguvu wa kati amefanikiwa kuteka hisia za mashabiki wa klabu hiyo ya London Kaskazini- akifanya kazi nzuri mwanzoni mwa msimu huu. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment