NAHODHA,MAOFISA JWTZ WAMUAGA MLIMA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga 
Taifa, Shamsi Vuai Nahodha jana aliwaongoza maofisa wa JWTZ katika kutoa
 heshima za mwisho kwa mwili wa Luteni Rajab Ahmed Mlima.
Marehemu Luteni Mlima, aliuawa akiwa 
katika Uwanja wa Mapambano na wanagambo wa Kundi la Waasi wa M23, katika
 Milima ya Gavana, karibu na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya 
Congo, wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Viongozi wengine walioshiriki katika 
kutoa heshima zao za mwisho kwa ofisa huyo, ni pamoja na waziri wa 
zamani katika wizara hiyo Profesa Philemon Sarungi, Mnadhimu Mkuu wa 
JWTZ Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na viongozi mbalimbali wa 
Serikali.(P.T)
            
Akizungumza na waandishi wa habari 
baada ya kutoa heshima hizo, Waziri Nahodha alisema Serikali inatoa pole
 kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, kwa kumpoteza
 mtu shujaa aliyekuwa akitetea roho za watu.
Alisema hata hivyo, Serikali haitarudi nyuma katika masuala ya ulinzi wa amani, na kwamba itaendelea kutoa msaada wa ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi hapo amani itakapopatikana.
"Kwa kweli tumepata pigo kubwa la kuondokewa na shujaa wetu, lakini sisi kama Serikali hatutarudi nyuma kwenye masuala ya ulinzi wa amani hadi pale tutakapoona amani imepatikana,"alisema Nahodha.
Waziri huyo alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kutoa msaada kwa familia ya marehemu Luteni Mlima, kwani hilo ni jukumu lake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Ndomba, alisema Luteni Mlima amefariki kishujaa wakati akilinda amani na kwamba siku zote jeshi litatambu mchango wake.
                    
No comments:
Post a Comment