RIPOTI YAONYESHA WIZI WA FEDHA WA KUTISHA
Taasisi za Fedha nchini zimepoteza
kiasi cha Sh34.4 bilioni kuanzia kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi
Oktoba mwaka huu kutokana na wizi wa fedha katika taasisi hizo,ripoti
mpya imebainisha.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi za
Kenya,Tanzania na Uganda umebainisha kuwa,Taasisi za Fedha za Afrika
Mashariki zimepoteza zaidi ya Sh471 bilioni sawa na (USD 30 milioni) kwa
mwaka.
Hata hivyo benki hizo ziliweka wazi
upotevu wa Sh126.9 bilioni tu ambao ni robo ya upotevu huo wa zaidi ya
Sh471 bilioni kwa kile kinachodaiwa kuhofia kupoteza wateja.
"Taasisi za fedha zinapoteza fedha
nyingi kutokana na teknolojia na watendaji wa ngazi za juu kuhusika kwa
kiwango kikubwa lakini hazitaki kukiri kwa sababu ya kuhofia kukosa
wateja," alisema Robert Nyamu, Mkurugenzi wa Delloite, Afrika Mashariki.(P.T)
Msemaji wa Benki Kuu ya Tanzania,Loy
Nabeta hakuwa tayari kuzungumzia upotevu huo na kusema kuwa ni suala
linalohitaji majadiliano ya kina na utendaji wa ngazi za juu.
Wimbi la wizi wa fedha katika benki lilianza kupata umaarufu mwaka 2010 na Oktoba 2012 hadi Februari 2013, inakadiriwa kuwa jumla ya Sh700 milioni zimeibwa katika benki mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Ripoti hiyo ya Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2013 iliyotolewa na Kampuni ya Uchunguzi wa Huduma ya Delloite imebaini kuwa watendaji wa ngazi za juu wanahusika zaidi na uhalifu huo ukilinganisha na watendaji wa ngazi za chini.
"Wanapofanya uhalifu hujua namna ya kuuficha na kuujadili na wasimamizi wa ndani bila kubainika.Wanajua mbinu na mifumo yote ya kifedha na wanatumia fursa hiyo kuiba," alisema Nyamu.
Watendaji waliotajwa kuhusika zaidi na wizi huo wa fedha ni wale wa ngazi za juu wakiwamo wakurugenzi watendaji, ofisa operesheni, wakurugenzi wa fedha, vitengo vya teknolojia na wakuu wa vitengo wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa fedha ukilinganisha na wafanyakazi wa kati na ngazi za chini.
Wizi unaofanyika zaidi katika nchi za Afrika Mashariki unatajwa kuwa ni wa fedha halali ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya uhalifu wa aina zote wa kifedha.
Hata hivyo Nyamu alisema watendaji wa ngazi za chini wanaweza kufanya uhalifu wa kiasi kikubwa cha fedha iwapo wanajua namna ya kufanya hivyo.
Mtaalamu wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM), Dk Eliamani Sedoyeka alisema ni kweli kuwa watu wa ngazi za juu wanatumia nafasi zao kufanya uhalifu wa kifedha kwa sababu wanaelewa kwa undani mfumo unavyofanya kazi na kutolea mfano i wizi wa Benki ya Stanbic .

No comments:
Post a Comment