NIDA:WATENDAJI WANAODAI FEDHA ZA VITAMBULISHO KUKIONA
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaonya baadhi ya watendaji wa mitaa
jijini Dar es Salaam wanaodaiwa kuwatoza fedha wananchi kwa ajili ya
kuwapatia vitambulisho hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua
za sheria.(HD)
Aidha,
imesema zoezi la utaoji wa vitambulisho limefikia katika hatua ya
kuchukua alama za vidole na picha kwa watu waliojaza fomu za kuviomba.
Mkurugenzi
Mkuu wa Nida, Dickson Maimu, akizungumza katika mahojiano na Radio One,
alisema zoezi la vitambulisho linagharamiwa na serikali kwa asilimia
100, hivyo hairuhusiwi mtendaji yeyote kumtoza fedha mwananchi.
Alisema
zoezi linaendelea katika wilaya za Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar na
kuwa wanaopuuza kupata vitambulisho vya taifa watapata athari ikiwamo
kushindwa kupata huduma mbalimbali kama kufungua akaunti au kupata
ajira.
Kuna
madai kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa katika jijini Dar es Salaam
wamekuwa wakiwatoza Sh. 2,000 watu wanaokwenda katika ofisi zao ili
kugongewa mihuli.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment