MILIPUKO NJE YA OFISI ZA CHAMA TAWALA CHINA
Msururu wa milipuko midogo nje ya afisi za kimkoa za chama tawala cha Kikomunisti,imesababisha kifo cha mtu mmoja
Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamesema kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu madogo yaliyotengenewa nyumbani.
Mlipuko huo uliotokea muda wa asubuhi wenye shughuli nyingi, ulisababisha kuvunjika kwa madirisha na moshi mkubwa kufuka.
Ripoti zilizotolewa na shirika la
habari la kiserikali zilisema kuwa mabomu madogo yalikuwa yamefichwa
ndani ya maua kando ya barabara.
Milipuko hiyo ilitokea Kaskazini mwa China katika eneo la, Tai-yuan, mkoani, Shanxi,(P.T)
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu 8 wamejeruhiwa na magari mawili kuharibiwa.
Picha zilizowekwa kwa mitandao ya
kijamii imeonyesha moshi ukifuka pamoja na magari ya wazima moto ikiwa
katika eneo la shambulizi ambalo lilitokea mapema asubuhi ya leo.
Hakuna taarifa za kina kueleza kiini
cha milipuko hiyo. Hata hivyo kumekuwa ma matukio ya mara kwa mara ya
wananchi kufanya mashambulizi kama haya dhidi ya serikali hasa wale
ambao hawahisi kuridhishwa na serikali hiyo.
Hali ya wasiwasi pia imetanda hasa
baada ya tukio la wiki jana mjini Beijing ambalo mamafisa walisema kuwa
lilikuwa njama ya shambulizi la kigaidi
No comments:
Post a Comment