M23 'WAMALIZA UASI 'BAADA YA KIPIGO

Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya 
Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo 
muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya 
serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa 
kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.(P.T)
Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi 
hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na 
makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao 
kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na 
kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri 
ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi
 yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda
 wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo 
yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa
 kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu
 na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda 
ambayo ni ngome yao muhim
No comments:
Post a Comment