KERRY AZURU MISRI
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
John Kerry amewasili Misri Jumapili kituo cha kwanza katika ziara yake
ya kidplomasia kwa siku 9 Mashariki ya Kati na Ulaya. Ziara ya Kerry
huko Cairo imefanywa siku moja kabla ya kesi dhidi ya rais aliyetimuliwa
madarakani Mohammed Morsi kuanza kesho Jumatatu. (HM)
Morsi alitimuliwa madarakani na majeshi mwezi Julai na kushtakiwa kwa makosa ya kuchochea mauaji ya waandamanaji waliokuwa nje ya kasri ya rais mwezi Desemba.
Utawala wa rais Obama umedhibiti baadhi ya msaada wa kila mwaka kwa jeshi la Misri ambao ulikuwa wa takriban dola bilioni 1.3 kutokana na umwagaji damu nchini humo na msukosuko wa kisiasa.
Kerry atakwenda Saudi Arabia baadaye leo Jumapili kwa mazungumzo na viongozi wa Saudia kuhusu Misri, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria na majadiliano juu ya program ya nuklia ya Iran.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani baadaye atakwenda Bethlehem ambako atakutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmud Abbas.Pia atazuru Jordan,Milki ya nchi za Kiarabu, Algeria,Morocco na Poland. Chanzo: voaswahili
No comments:
Post a Comment