TANAPA YAJIKITA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI

Mkurugenzi
 Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akielezea kwa waandishi 
wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema hii leo juu ya 
mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga 
maeneo 34 ya uwekezaji, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari 
(MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.

Baadhi ya
 waandish wa Habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi 
za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakati akielezea mikakati ya kuinua 
utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya 
uwekezaji.
Picha na Eliphace Marwa, MAELEZO (P.T)
Hifadhi ya Serengeti ni moja kati ya maajabu Saba Barani Afrika.

Hifadhi ya Mikumi inapatikana Mkoa wa Morogoro

Hifadhi za milima Udzungwa inapatikana katika mkoa wa Morogoro ni moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) 
limetenga maeneo 34 kwa ajili ya uwekezaji katika huduma za malazi kwa 
wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi mwa nchi kwa ajili 
ya utalii.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es 
salaam na Mkurugenzi mkuu wa TANAPA bw. Allan Kijazi wakati akizungumza 
na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya shirika hilo kupanua Sekta ya 
utalii hapa nchini hasa kwa kupanua huduma za 
malazikatikahifadhizaKilimanjaro,Katavi,Mikumi,Mkomazi,Ruaha,Saadani,tarangire,Rubondo
 na Kitulo.
Akifafanua zaidi bw. Kijazi alisema 
lengo la Tanapa ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyotengwa yanapata 
wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kutafanyika kongamano 
maalum mwezi Februari 2014.
Bw. Kijazi alisema kuwa kongamano hilo
 litawaleta pamoja wakezaji wakubwa na wadogo ambao watapata fursa ya 
kuyafahamu maeneo hayo na namna gani uwekezaji wao utakavyoleta faida 
kwa sekta ya utalii na uchumi nchini.
Aidha Bw. Kijazi alisema kwamba 
vitanda katika maeneo ya hifadhi kwa sasa kuna vitanda 6,681 ambapo kwa 
miaka mitano ijayo idadi hii itafikia vitanda 8,421.
Aliweka bayana kuwa uamuzi wa TANAPA 
kutenga maeneo mapya ya uwekezaji umezingatia ukuaji wa sekta ya utalii 
nchini ambapo karibu asilimia 75 ya wageni wanaofika nchini ni watalii.
Baadhi ya vivutio vinavyoifanya 
Tanzania kuongoza katika Afrika na Dunia katika Sekta ya utalii ni 
pamoja na Hifadhi za Taifa Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire.
Vivutio vingine ni Ziwa manyara, Arusha,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na pori la Akiba la Selous.
Mwisho
No comments:
Post a Comment