TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, November 15, 2013

SMZ YAANDAA MASHINDANO YA MICHEZO YA 17 KUHADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

zanznoibar_bb026.jpg
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Ali Mbaruk akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu michezo mbalimbali itakayofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo adhimishwa Mwezi January 2014,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)(P.T)
Frank Mvungi - Maelezo
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeandaa mashindano ya michezo 17 kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi hayo itakayofikia kilele januari 12,2014 ambayo ni siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari , Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Mh. Said Ali mbaruk wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya michezo ya kuadhimisha mapinduzi hayo.
Mh. Said Ali Mbaruk amesema kuwa katika kuadhimisha mapinduzi hayo michezo mbalimbali itafanyika ikiwemo mpira wa miguu,riadha,volleyball,Table tenis na mazoezi ya viungo.
Akifafanua zaidi Alisema michezo hiyo pia itawahusisha watu wenye ulemavu ambapo kwa kushirikiana na Kamisheni ya utalii michezo mingine itakayofanyika ni karata,bao,squash na kuogelea .
Akieleza zaidi Mh. Said Ali Mbaruk aisema kuwa katika michezo hiyo kutakuwa na timu zaZanziba,Tanzania bara,Afrika Mashariki,ambapo mashindano hayo yanapata hadhi ya kimataifa.
Pia alizitaja timu zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni Azam FC,Simba, Yanga,Mbeya city kwa upande wa Tanzania bara, baadhi ya timu toka Zanzibar ni chuoni,Pemba combine na Unguja combine.
Katika maadhimisho hayo mechi zote zitatangazwa moja kwa moja kupitia ZBC TV,kwa kushirikiana na Azam TV.

No comments:

Post a Comment