MOYES AWATAKA MAREFA KUMLINDA JANUZAJ KAMA MESSI
KOCHA David Moyes amesema winga Adnan 
Januzai lazima alindwe na marefa baada ya Sascha Riether kuwa mchezaji 
wa kwanza kuadhibiwa chini ya sheria mpya baada ya marefa kutoona tukio 
uwanjani. (HM)
        
Mshambuliaji huyo kinda alikuwa alichezewa rafu na beki huyo wa Fulham, United ikishinda 3-1 Uwanja wa Craven Cottage Jumamosi.
Refa Lee Probert na wasaidizi wake hawakuona tukio hilo wakati linatokea, lakini marudio ya picha za video yanaonyesha vizuri.
Na kwa sababu huyo, beki huyo wa pembeni ameadhibiwa na FA kwa kufungiwa mechi tatu.
Inamaanisha Riether anakuwa mchezaji wa kwanza kuadhibiwa chini ya sheria mpya ya FA, kumuadhibu mchezaji ambaye alifanya kosa lakini halikuonekana kwa marefa wakat wa mechi. Chanzo: binzubeiry

No comments:
Post a Comment