MAKINDA AAMUA ‘UGOMVI’BAINA YA LUKUVI, ABWAO
Spika wa
Bunge, Anne Makinda jana aliingilia kati mvutano baina ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
baada ya kubanwa na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Chiku Abwao.
Hali hiyo
ilijitokeza pale Lukuvi alipolazimika kutumia nafasi yake ya uwaziri
kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Abwao kuhusu mpango wa serikali
wa kufikisha maji Isimani. "Mheshimiwa Waziri, Jimbo la Isimani
wananchi wake wana matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji na wamekuwa
na maisha magumu,hivyo wanahitaji msaada huo, je Serikali inatoa kauli
gani kuhusu kuwasaidia wananchi hao," aliuliza Abwao.(P.T)
Akijibu
swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen
Wassira alisema shida waliyonayo wananchi wa Isimani ni sawa na maeneo
mengine nchini .
Baada ya
majibu hayo, Lukuvi alilazimika kusimama ghafla na kuwasha kipaza
sauti,ili kusawazisha jibu la swali hilo ambalo lililenga moja kwa moja
katika jimbo lake,Baadhi ya wabunge walianza kupiga kelele za kumtaka
Lukuvi asizungumze kwa kuwa swali lilimlenga moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment