Dr. SENGONDO MVUNGI AMEFARIKI DUNIA HOSPITALINI SOUTH AFRIKA

Ni
 jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza
 kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi uliofanywa
 dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya 
Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Taarifa iliyotumwa millardayo.com inasema Dr Mvungi amefariki dunia 
akiwa mahututi hospitalini nchini Afrika Kusini muda mfupi uliopita na 
taarifa kutumwa nyumbani Tanzania ambapo wafanyakazi wenzake ofisi ya 
tume ya mabadiliko ya katiba wameambiwa wakae karibu na simu zao ili 
kikitokea chochote kingine wafahamishwe.
Tayari viongozi mbalimbali kama Mh. Warioba, Katibu wa tume, naibu na
 watumishi wengine wachache wamekwenda nyumbani kwa marehemu.
No comments:
Post a Comment