TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 17, 2013

NAPE AKWEPA KUZUNGUMZIA MATOKEO UDIWANI ARUSHA..."WAULIZENI VIONGOZI WA CCM ARUSHA"


Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa jambo lolote linalohusu uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika Jumapili wiki iliyopita, jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa huo.

Nape alisema hayo alipozungumza na Nipashe  jijini Dar es Salaam jana, baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne.

“Waulize wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua chama chetu kimegawa majukumu. Kule kuna mwenyekiti wa mkoa, katibu pamoja na wengineo,” alisema Nape.


Alipoulizwa sababu  za kutoa maoni katika chaguzi nyingine mara tu matokeo yanapotangazwa, kama vile Jimbo la Igunga, Nape alisema uchaguzi huo unahusu ubunge  tofauti na udiwani.

Alisema hata katika uchaguzi wa kata nyingine 22, alizungumza kwa kuwa ulikuwa umehusisha kata mbalimbali nchini na siyo mkoa mmoja.

No comments:

Post a Comment