MASHAHIDI WAWILI WAJIONDOA KESI YA KENYATTA
KIONGOZI
wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, amesema
kuwa mashahidi wawili wametupilia mbali ushahidi wao katika kesi dhidi
ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Bi Bensouda alisema mashahidi nambari 5 na 426 wamefutilia mbali ushahidi wao kwa sababu za waswasi kuhusu usalama wao.
"kwa kifupi, inaonekana kuwa wasiwasi
wa shahidi nambari tano, wameogopa sana kuhusu usalama wao na kuwa
athari za kutoa ushahidi wake huenda zikawa na madhara makubwa kwa
maisha yake na kwa hivyo akaamua kufutia mbali ushahidi wake.'' alisema
Bensouda kwa ujumbe wake kwa majaji mnamo Jumanne. (HM)
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka,
ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili
msimamo wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.
"upande wa mashtaka umefanya mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, '' aliongeza kusema Bi Bensouda said.
Hata hivyo mwendesha mashtaka aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa.
Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza kusikilizwa Novemba 12. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment