WAFUASI WA MORSI WAENDELEA KUPIGA KAMBI
WAFUASI wa Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya mashariki mwa mji mkuu wa Cairo,
Ikiwa ni siku moja tu baada ya ghasia kali kuzuka.
Waandamanaji hao wameweka vizuizi
katika kambi yao na kuapa kutoondoka licha ya mapambano kati yao na
vikosi vya ulinzi na usalama.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesitikitishwa na ghasia zinazoendelea nchini Misri. (HM)
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari,bwana Kerry amesema kuwa wakati huu ni muhimu sana kwa taifa hilo
na akatoa wito kwa serikali hiyo kuheshimu haki ya raia kuandamana kwa
amani na uhuru wa kujieleza.
Mwandishi wa BBC anasema hali sasa imetulia kiasi licha ya vurugu kutokea katika viunga vingine vya mji wa Cairo. Chanzo: bbcswahili
Mwandishi wa BBC anasema hali sasa imetulia kiasi licha ya vurugu kutokea katika viunga vingine vya mji wa Cairo. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment