TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, July 20, 2013

CHRIS BROWN JELA TENA!
LOS ANGELES, Marekani
STAA wa muziki, Chris Brown huenda akachezea miaka kadhaa jela endapo mahakama ikimkuta na hatia.
Mapema wiki hii, mwanamuziki huyo alifikishwa katika mahakama ya mjini hapa kujibu tuhuma ya kugonga na kukimbia miezi miwili iliyopita.

Brown ambaye aliwahi kufungwa kutokana na kumpiga zilipendwa wake, Rihanna alipofikishwa mahakamani hapo mapema wiki hii, alitakiwa kujibu kesi ya kugonga na kukimbia pamoja na kukutwa bila ya kuwa na leseni siku ya tukio.
Kabla ya kupandishwa kizimbani, Brown alifikishwa mahakamani hapo mwezi uliopita na jalada lake likasogezwa mbele hadi Jumatatu ya wiki hii.
Mawakili wa staa huyo walimtetea,  akaachiwa kwa dhamana na shauri lake litatajwa tena Agosti mwaka huu na endapo akipatikana na hatia, atahukumiwa jela kulingana na vifungu vya sheria vya nchi hiyo.


No comments:

Post a Comment