DRC: M23 WADAI KUMSHIKA MATEKA MTANZANIA
KUNDI
 la waasi la M23 nchini Drc limedai kumkamata mtu mmoja aliyetambulishwa
 kwa jina la Christopher George Yohana katika hati yake ya kusafiria 
akipigana sambasamba na  jeshi la serikali FARDC kupambana na kundi la 
M23 katika maeneo ya kibati nchini DRC.Msemaji wa kundi la M23 Vernnei Kazarama ameiambia sauti ya amerika kwa njia ya simu kwamba kijana huyo anayesadikiwa kuandikishwa na serikali ya congo kama mwanajeshi wa Tanzania amejieleza na kukubali kwamba anatokeo nchi jirani ya Tanzania. (HM)
            
 Mapigano yenye ghasia kubwa 
yalitawala Jumatatu ikiwa ni mwendelezo wa ghasia za mapigano mapya 
yaliyozuka julai 10 huko kivu kaskazini na kulazimisha maelfu ya watu 
kukosa makazi na kutorokea nchi jirani ya Uganda.
Kazarama amesema kama serikali ya Tanzania itaomba kuachiliwa mwanajeshi huyo kutoka tanzania kwa njia ya kipiplomasia au kupitia shirika la msaba mwekundi M23 iko radhi kumwachilia huyu mateka huyo.
Hata hivyo ameishutumu nchi ya Tanzania akisema kuwa imekuwa ikiruhusu wapiganaji kutoka Tanzania kusaidiana na vikosi vya serikali ya Congo badala ya wale wa ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa.
Jumatatu kundi la M23 ilisambaza hati ya kusafiria yenye majina kamili na utaifa wa mateka huyo ikidai kwamba inataka kutuma ujumbe kwa dunia nzima kwamba Tanzania inaisadia Drc katika uvunjifu wa amani.
Sauti ya ameriba bado inaendelea kuitafuta serikali ya tanzania ili kutoa ufafanuzi zaidi juu ya maelezo yaliyotolewa na kundi la waasi la M23.Chanzo: voaswahili
                    
No comments:
Post a Comment