CHINA KUSHIRIKIANA NA CCM KATIKA UJENZI WA CHUO CHA IHEMI IRINGA
SERIKALI 
ya nchi ya China imekusudia kushirikiana na chama cha mapinduzi (CCM) 
katika kufufua chuo cha vijana Ihemi katika wilaya ya Iringa mkoani 
Iringa kwa ajili ya kukiwezesha chuo hicho kutoa mafunzo ya uongozi kwa 
vijana kutoka nchi za Sadac pamoja na nchi ya China .
Katika 
kuonyesha mikakati ya awali ya kuanza kukifufua chuo hicho balozi wa 
chini nchini Tanzania Bw Lu Youqing leo amekitembelea chuo hicho chenye 
eneo la ukubwa wa hekari 1900 na kuonyesha kuvutiwa zaidi na eneo hilo.
Akielezea
 mkakati huo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye 
alisema kuwa CCM inaompango wa kukiendeleza chuo hicho kwa kushirikiano 
na serikali ya China .
"Leo 
tumekuja na balozi wa China kwa ajili ya kupaendeleza zaidi ikiwa ni 
pamoja na kutoa elimu ya uongozi pamoja na masuala ya ujasiriamali 
ambayo yatawafanya zaidi vijana kuweza kujiajiri zaidi"
Alisema 
kuwa mpango wa kukifufua chuo hicho unataraji kuanza mara moja na kuwa 
hayo ni maamuzi ya mkutano mkuu wa Taifa ambayo utekelezaji wake unaanza
 mara moja .
Nnauye 
alisema kuwa kutokana na maamuzi hayo ya mkutano mkuu wao wameanza 
kufanyia kazi suala hilo kwa kuwatafuta wahisani hao kutoka China ambao 
watasaidia kufanikisha ujenzi huo ambao kukamilika kwake ni ukombozi 
mkubwa kwa vijana nchini nan chi nyingine .
Pia 
alisema kuwa kuyumba kwa chuo hicho kunatokana na mfumo wa vyama vingi 
na kuwa kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza chuo hicho cha Ihemi 
kilikuwa kikifanya kazi vema japo alisema kwa sasa mkakati ni kukifufua 
na kuwa chuo hicho kitakamilika ndani ya mwaka huu .
Kuhusu 
aina ya mafunzo yatakayotolewa alisema kwa sasa ni mapema sana ila mara 
baada ya ujenzi kukamilika basi aina ya mafunzo yatakayotolewa 
yatajulikana .
Nnauye 
alipoulizwa kuhusu gharama ya jumla itakayotumika kujenga chuo hicho 
alisema kuwa kwa sasa bado ni mapema kujua ni kiasi gani kitatumika 
katika ujenzi na kuwa hatua iliyopo sasa ni ya awali zaidi .
Katika 
ziara hiyo ya balozi wa China nchini aliongozana na msaidizi wake 
Bi.Wang Fang pamoja na katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana 
,katibu mkuu wa UVCCM Taifa Martine Shegela pamoja na viongozi mbali 
mbali wa chama na serikali wilaya na mkoa wa Iringa .
No comments:
Post a Comment