TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, July 20, 2013

SELENA GOMEZ AANZA KUJITEGEMEA
NEW YORK, Marekani
MWANAMUZIKI Selena Gomez anatarajia kuanza kununua mjengo wake na kuanza maisha ya kujitegemea.
Kabla ya kupata wazo la kuondoka nyumbani, Selena mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akiishi na mama yake mzazi pamoja na baba wa kufikia ambaye pia ana watoto wake.
Akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha American Idol juzikati, Ryan Seacrest, Selena alionesha wazi dhamira yake ya kuanza maisha ya kujitegemea.
“Ndiyo, unajua… nafikiri ndiyo muda muafaka. Napenda kuishi pamoja na familia yangu niliyoizoea lakini muda umefika na mimi napaswa kuwa na mji wangu,” alisema Selena pasipo kuweka wazi eneo analotaka kuhamia.

No comments:

Post a Comment