Mhe Makamba mgeni rasmi semina ya usalama wa matumizi ya kompyuta

Na:Lorietha Laurence-Maelezo
Taasisi 
huru isiyo ya kiserikali kutoka nchini Marekani inayoitwa ISACA tawi la 
Tanzania kwa kushirikiana   na kampuni ya Norway inayoshughulikia 
maendeleo Afrika Mashariki (Norway Registers Development  East Africa 
Limited –NRD-) wameandaa semina  ya usalama wa matumizi ya  kompyuta na 
mitandao yake katika nyanja mbalimbali kwa mashirika ya umma, benki, 
serikali na watu binafsi.Semina hiyo 
        
                        
        
        
        
 inayotarajiwa
 kufanyika Agosti 28 hadi 30  mwaka huu katika Hoteli ya Nashera mkoani 
Morogoro ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Mhe 
January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  .
Akizungumza
 na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam Rais wa ISACA Bw. 
Boniface Kanemba ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana 
na   ongezeka la wizi wa mitandao  na matumizi mabaya ya mitandao 
uliojitokeza katika miaki ya hivi karibuni.
“Mafunzo 
haya ni kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka sekta zote za umma na 
binafsi  pia kutoka nchi zote tano za Afrika Mashariki zikiwemo, 
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kutokana na nchi hizi kuwa na
 changamoto sawa  na ongezeko la wizi wa mitandao “alisema Kanemba.
Rais huyo
 wa ISACA ameongeza kuwa changamoto kubwa ya wizi wa mitandao inatokana 
na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya simu katika kutuma na kupokea 
pesa.
Hivi 
karibuni, makampuni ya simu yamekuwa yakitumia mtandao mfano M-pesa na 
Tigo Pesa kutuma hela kwa wateja ambapo kumekuwa na kesi nyingi za wizi 
kwa kutumia miamala hiyo pamoja na upotevu wa nyaraka muhimu 
za makampuni binafsi ,umma na Serikali.
Naye 
Mkurugenzi Mtendaji wa NRD East Afrika Sebastian Marondo akizungumzia 
umuhimu wa semina hiyo amesema, “sio jukumu la serikali peka yake 
kupambana na uhalifu bali ni jukumu la kila mwananchi ,makampuni na 
mashirika binafsi katika kulinda  na kujenga nchi yetu.”
ISACA ni 
taasisi huru ya kimataifa   isiyokuwa ya faida  inayohusika  katika 
kusimamia na kutoa mafunzo na maarifa ya mifumo ya mitandao wakati NRD 
East Afrika  ni kampuni inayojihusisha na mifumo ya mitandao ya kompyuta
 na usalama wake.
No comments:
Post a Comment