MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AIONYA CHADEMA
Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa
wanachama na viongozi wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya
nchi badala ya kutumia uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta
mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.
Pia
amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa
vijana wake nchi nzima.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili
wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA
au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya
kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.
Anaongeza
kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini
hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda
kama walivyo tangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na
Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Nyahozo
ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika
Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya
mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu
yao.Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo
sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au
watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo sema.
“Hakuna
maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu
kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama.Ni vyema
wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa
Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman
utulivu na umoja wa Kitaifa”, alisema Nyahoza.
Alisema
kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa “Bila kujali masharti ya ibara ya
(1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa
ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani
matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa.
Nyahoza
alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza
wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi
nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo
watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
No comments:
Post a Comment