TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, July 20, 2013

YATIMA WANAHITAJI MSAADA

KITUO cha watoto yatima cha Yatima Islamic, kinaomba msaada kwa wasamaria
wema kukisaidia pango la nyumba.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kituohicho kilichopo Buguruni Ally Hamza, Rashid Akungwa alisema kuwa, wanadaiwapango zaidi ya sh. milioni nne, baada ya awali waliyolipiwa na mhisani kuisha muda
wake.
"Awali alijitokeza mtu ambaye, aliona mazingira ya watoto, kwamba tulikuwa katika nyumba ya vyumba viwili, na watoto ni wengi..ndipo alipotutafutia sehemu hii na
kutulipia kodi ya mwaka ambayo imeshamalizika tangu mwezi uliopita,"aliongeza.
Alisema kwa sasa wana hali mbaya, na endapo watafukuzwa katika nyumba hiyo,
basi watoto hao zaidi ya 50, huenda wakakosa pa kwenda na hatimaye kuzagaa
mitaani.
Watoto wengi wanaoishi katika kituo hicho wana umri kati ya miaka minne hadi 15,ambapo wengi wanasoma shule ya msingi, huku mmoja aliyekuwa akisoma
sekondari, amemaliza.
Katibu wa kituo hicho, Aboubakary Simba, alisema mahitaji mengine ni pamoja na
futari na daku hasa kwa mwezi huu wa Ramadhani, mavazi kwa ajili ya watoto na mahitaji ya kawaida ya kibinadamu.
Alisema msaada wa aina yeyote wenye hadhi na utu, unapokelewa na kwa yeyote ataliyeguswa kuchangia anaweza kupata maelezo kupitia namba 071 03 8888 au
0712150928.

No comments:

Post a Comment