YANGA,URA WATOKA SARE 2-2

 Mshambuliaji wa URA akijaribu kuwatoka mabeki wa Yanga (HM)

MABINGWA wa soka Tanzania bara, klabu 
ya Yanga angalau jana wamepata cha kusema baada ya kupata sare ya 2-2 
dhidi ya Wakusanyaji wa Mapato wa nchini Uganda, klabu ya URA, katika 
mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar 
es salaam.
Yanga waliponea chupuchupu kulala kama
 wenzao Simba siku ya jana ambapo waliburuzwa 2-1 na wakali hao wa 
Uganda, lakini mshambuliaji ambaye hajaifungia Yanga kwa muda mrefu, 
Jerryson Tegete aliwapa cha kusema mashabiki wao baada ya kusawazisha 
bao la pili dakika ya 90 ya kipute hicho.
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema Yanga walicheza vizuri kipindi cha pili, lakini kipindi cha kwanza URA walitawala zaidi mchezo wakipiga soka la uhakika.
Kizuguto alisema kocha wa klabu hiyo 
Ernie Brandts amesisitiza kuwa kikosi chake kimecheza vizuri, lakini 
wapinzani wake walikuwa wazuri sana.
Afisa habari huyo alisema kesho kikosi
 hicho kitakuwa na mapumziko, na kesho kutwa jumanne kitaendelea na 
mazoezi yake katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Loyola mabibo jijini
 Dar es salaam.
“Mechi ya leo ilikuwa nzuri sana kwa 
kikosi chetu, kocha amewapima wachezaji wake mbele ya timu nzuri, lakini
 sisi bado timu yetu ni nzuri sana”. Alisema Kizuguto.
Pia alisema hamasa ya mashabiki wa 
Yanga uwanjani imeonesha kuwa wanaipenda timu yao na wanatakiwa kuwa na 
moyo wa kuipenda zaidi kwani itawapa raha.
“Yanga ni timu ya wananchi,na ndio 
maana kila inapocheza wananchi wanajitokeza kwa wingi, hakika 
hatutawaangusha hata kidogo”. Alisema Kizuguto
No comments:
Post a Comment