VIJANA WAASWA
Waziri
wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara
akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na
inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia
imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth
Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo.
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana
wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo
pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Na Frank Shija - Maelezo
Vijana
nchini wameaswa kujitambua na kuthubutu kwa malengo chanya pamoja ikiwa
ni pamoja na kujituma kufanya kazi zikiwemo za kujitolea kwa kuwa kwa
kufanya hivyo wataweza kujikwamua na kujiletea maendeleo yao na Taifa
kwa ujumla..
Rai hiyo
imetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenella
Mukangara alipokuwa akifungua kambi ya dunia ya vijana leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Fenella amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoe na kufuata
mikomba ambapo ni hatari sana matokeo yake wamekuwa wakijikuta
wakitenda tofauti na malengo yao.
Aliongeza
kuwa ni wakati sasa kwa vijana kujitambua na kubadilisha fikra zao hili
waweze kujiletea maendeleo wao wenyewe baadala ya kulalamika kama
ambavyo wamekuwa wakifanya.
"Ni
muhimu vijina mjitambue na mthubutu kwa malengo chanya, na muanze kwa
kila mmoja wenu kujituma kufanya kazi na wakati mwingine jitoleeni kwa
faida ya jamii zenu". Alisema Waziri Fenella
Aliongeza
kuwa Mungu amewajali vijana Talanta na vipaji tofauti hivyo ni muhimu
vikatumika kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla na
kuongeza kuwa kujitambua kwa vijana kuendane na uthubutu ili kujikwamu
kimaendeleo.
Kwa
upande wake mwanzilishi wa IYF duniani Pastor Park Ock Soo amesema kuwa
ni faraja kwake kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki kambi hiyo
akiamini malengo ya kuanzishwa kwa taasisi yake yamefikiwa kwa kiasi
kikubwa.
Pastor
Park ameongeza kuwa vijana wanapaswa kubadili fikra na mitazamo yao ili
kuenenda na kasi ya kujiletea maendeleo badala ya kulalamika na kusubiri
kufanyiwa kazi.
Kambi hii
ya vijana ni inafanyika hapa nchini kwa mara ya tano na imeandaliwa na
taasisi ya International Youth Fellowship (IYF) kutoka Korea kwa
kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ni "Badilisha Fikra ktuoka mtazomo hasi kuw
chanya"
No comments:
Post a Comment