KIUNGO WA AZAM HUMPHREY MIENO ATAJWA KWENDA CELTIC

VICTOR Wanyama ameondoka Celtic 
Football Club na kujiunga na klabu inayoshiriki kwenye ligi kuu ya 
England - Southampto baada ya kukamilisha uhamisho wa wa 
£12.5million.(HM)
Sasa ikiwa ni wiki kadhaa tangu kiungo
 huyo wa Kenya kuondoka, kocha wa Celtic Neil Lennon, amesema Wanyama 
alikuwa ndio kiungo wake bora wa ushambuliaji kwenye timu yake na sasa 
wanahitaji mbadala wake. 
Kutokana na hilo sasa zimeibuka 
taarifa kwamba kocha huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa Celtic 
anamuwania kiungo mwingine kutoka Kenya Humphrey Mieno. Mieno ambaye kwa
 sasa ni mchezaji wa Azam FC  inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Tanzania. 
Celtic, itabidi ifanye haraka kumsaini
 mchezaji huyo wa Azam FC kwa kuwa kuna vilabu vingi barani Afrika kama 
miamba ya soka ya Tunisia Esperance na Club Africain zinamuwania kwa 
nguvu mchezaji huyo ambaye alihamia Azam akitokea Sofapaka ya Kenya.
No comments:
Post a Comment