MKOA WA RUKWA KUJENGA CHUO KIKUU

Jennifer Chamila-Maelezo
MKOA wa 
Rukwa unatarajia kuanzisha chuo kikuu ambacho kitasaidia vijana wengi 
wanaokosa nafasi za kuendelea na elimu ya juu kwa kupata nafasi ya 
kujiunga na chuo kikuu.
Mkakati 
huo unaosimamiwa na Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa(JUMARU) ambao ni 
halali chini ya sheria za nchi ilioanzishwa mwaka 2009 na wakazi wa mkoa
 wa Rukwa(Wanarukwa) kwa lengo la kuunganisha nguvu za wanarukwa wote 
ili kuleta maendeleo katika mkoa huo na wakazi wake.
        
Akiongea 
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa 
Sekretariati wa JUMARU Bw.Joachim Sikulumbwe amesema kuwa wameandaa 
kongamano la wanarukwa wote waishio jijini Dar es Salaam litakalo 
fanyika Septemba 01 mwaka huu,katika ukumbi wa Ubungo –Urafiki Social 
hall.
"Kongamano
 hilo litazungumzia maliasili na rasilimali za mkoa wa Rukwa na 
maendelao yake ,kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni nawaomba 
wanarukwa wajitokeze na kuhudhuria kwa wingi"alisema bw. Sikulumbwe,
Naye 
Makamo mwenyekiti kamati ya wahadhiri mchakato wa chuo kikuu cha Rukwa 
bw.Bernard Kasimila amesema sababu ya kuanzisha chuo hicho ni kuwezesha 
vijana wenye sifa za kuendelea na masomo kupata fursa ya kujiunga na 
chuo kikuu.
Mkoa wa 
Rukwa ni sehemu ya Tanzania iliyoko nyanda za juu kusini yenye wakazi 
zaidi yawakazi milioni moja kwa sense ya 2012 , una wilaya 3, 
halmashauri 4,tarafa 17,kata 64,na vijiji 202,unajishughuli zaidi na 
kilimo,uvuvi na utalii.
Mwisho
No comments:
Post a Comment