BALAZA KUU LA USALAMA UN LAJADILI USALAMA WA WAANDISHI
Bw.
Richard Engel kutoka NBC News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa
na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kueelezea uzoefu wao na mikikimikiki
wanayokumbana nayo wanapotekeleza majukumu yao ya kiuandishi. Bw. Engel
ambaye amesema amewahi kutekwa, alilitaka Baraza Kuu la Usalama
linapojadiliana kuhusu dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia
ni nani hasa mwandishi wa habari anaye stahili ulinzi na akahoji kama
wanaharakati ambao nao wanachukua picha za matukio mbalimbali na
kuzipost kwenye blog kama nao ni waandishi wa habari. pembeni yake ni
Bi. Kathleen Carroll, ambaye ni mhariri mtendaji wa Associated Press na
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kulinda Waandishi ( CPJ) yeye
katika mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza
maisha wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini
waandishi watano kati ya sita wanauawa ndani ya nchi zao wakati
wakitimiza majukumu yao.
No comments:
Post a Comment