TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 24, 2013

GERARDO MARTIN KOCHA MPYA WA BARCELONA

barce 8b63e
FC Barcelona imefikia makubaliano rasmi kumsaini Gerardo Martino kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FC Barcelona. (HM)
 Kilichobakia kwenye makubaliano hayo ni kusaini mkataba baada pande zote mbili kukubalina kila kitu.
Ratiba rasmi ya kuwasili kwake Nou Camp, utiaji saini wa mkataba na kutambulishwa rasmi itatangazwa msaa kadha yajayo. 
Gerardo ambaye anajulikana kama ‘Tata’, alizaliwa jijini Rosario (Argentina) November 20, 1962. Ana uzoefu mkubwa wa soka la America ya Kusini, kwanza kama mchezaji na baada kama kocha, kazi yake ya mwisho ilikuwa kuiongoza klabu ya Newell's Old Boys, ambao alishinda nao ubingwa wa mwaka huu.

Gerardo Martino anakuwa kocha wa nne raia wa Argentina kuifundisha FC Barcelona baada ya Roque Olsen, Helenio Herrera na César Luis Menotti.

MJUE GERARDO MARTINO

1962: Alizaliwa Novemba 20 mjini Rosario, Argentina.
1980-90: Kiungo huyo mshambuliaji anajiunga na Newell Old Boys ya Argentina na kuichezea mechi 392 za ligi, akifunga mabao 35 ndani ya miaka 10. Alitwaa taji la Primera pision mwaka 1988.
1991: Alicheza mwaka mmoja Tenerife na kuichezea mechi moja timu ya taifa yaArgentina chini ya Alfio Basile.
1991-94: Alirejea Newell Old Boys kwa miaka mitatu na kutwaa mataji mawili zaidi ya Argentina.
1994-95: Aliichezea kwa msimu mmoja Lanus kabla ya kurejea Newell Old Boys.
1996: Alikwenda Ecuadorian kuichezea mwaka mmoja Barcelona Sporting Club na kisha O'Higgins ya Chile.
1998: Alifanya kazi ya ukocha kwa mara ya kwanza Brown de Arrecifes.
1999: Alijiunga na Platense kama kocha.
2000: Alikuwa kocha Mkuu wa Instituto.
2002-03: Aliiongoza Libertad kutwaa mataji mawili ya Paraguay.
2004: Alitwaa taji la Paraguay akiwa na Cerro Porteno.
2005: Alikuwa kocha wa Colon kwa msimu.
2005-06: Alirejea Libertad na kutwaa taji la nne la Paraguay mwaka 2006.
2007: Februari - alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Paraguay na akashinda tuzo ya Kocha bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2010: Juni - Aliiongoza Paraguay katika Kombe la Dunia Afrika Kusini na kuifikisha hadi Robo Fainali, ambako ilifungwa na Hispania.
2011: Baada ya Paraguay kufungwa katika Fainali ya Copa America na Uruguay, ajajiuzulu ukocha wa timu hiyo ya taifa.
2012-13: Alirejea Newell Old Boys kama kocha na kutwaa taji la Clausura mwaka 2013.
2013: Julai 23 - Anakubali Mkataba wa miaka miwili Barcelona, kurithi mikoba ya Tito Vilanova.

No comments:

Post a Comment