MAPIGANO YAANZA TENA MJINI GOMA
MAPIGANO makali yameanza tena Mashariki mwa mji wa Goma katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo .
Mapigano hayo ni kati ya jeshi na wawaasi wa kundi la wapiganali la M23.
Makabiliano yalitokea katika kijiji cha Kanyanja umbali wa kilomita kumi na nne Kaskazini mwa Goma.
Pande zote mbili zimetuhumiana kwa kuanza mashambulizi kufuatia siku nne za mapigano wiki jana.
Kundi la M23 liliuteka kwa muda mji wa Goma Novemba mwaka jana ingawa waasi hao waliondoka baada ya mazungumzo ya amani ambayo kwa sasa yamedumaa. (HM)
Katika makabiliano yaliyotokea wiki jana , jeshi liliwafukuza waasi kutoka Goma ingawa hawakwenda mbali sana.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AF, mapigano yalikuwa makali sana huku makomboya yakitumika. Indaiwa ni waasi waliaonza vita kuwan kushambulia kambi ya jeshi ingawa madai hayo bado hayajathibitishwa.
Msemaji wa kundi hilo amekanusha madai hayo kuwa waasi ndio waliaonza vita. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment