TAIFA STARS YAWASILI KAMPALA KUIKABILI THE CRANES
Wachezaji wa Stars wakitua Kampala (HM)
TIMU ya Taifa (Taifa Stars) imewasili
Uganda jana jioni tayari kuikabili Uganda Cranes kwa mechi ya marudiano
kutafuta tiketi ya kucheza katika mashindano ya CHAN.
Kikosi hicho chichi nye wachezaji
20, kiliwasili muda mfupi baada ya saa kumi alasiri huku wachezaji na
benchi la ufundi wakiwa na matumaini makubwa.
Akiongea mara baada ya kuwasili Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen alisema wamejiandaa vizuri wakiwa
Mwanza na ana imanikikosi hiki kitabadili matokeo ya awali ambapo Stars ilifungwa 1-0 na Cranes Jijini Dar es Salaam.
Alisema licha ya kuwakosa wachezaji
Shomari kapombe na Mwinyi Kazimoto, ana imani na kikosi chake hiki kuwa
kitafanya makubwa Kampala.
“Tumekuja kubadilisha mahesabu kwani tumejiandaa vizuri kabisa,” alisema Poulsen.
“Tumekuja kubadilisha mahesabu kwani tumejiandaa vizuri kabisa,” alisema Poulsen.
Wadhamini wa Stars, Kilimanjaro
Premium Lager wamewaomba watanzania wasikate tama kwani Stars bado ina
nafasi kubwa ya kupindua meza.
“Sisi kama wadhamini bado tuna imani
na Stars na tunajua watatuwakilisha vizuri ni vyema watanzania wawe na
imani na kuiombea dua timu iibuke na ushindi mnono katika mechi hii ya
marudiano,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, george
Kavishe.Mechi hii ni gumzo kubwa Jijini Kampala kwani baadhi ya waganda wana hofu kuwa henda wakafungwa nyumbani kwao.
Mechi hii itapigwa katika Uwanja wa Nambole Jijini Kampala JUmamosi hii saa kumi jioni.
Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kufanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini
No comments:
Post a Comment