TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, July 8, 2013

MOURINHO ABADILI MFUMO WA UCHEZAJI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO
jose 2dd5f
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho (HM)
 jose2 c6ea1
Mourinho akiwa na wachezaji
jose3 32a06
KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba yuko tayari kumaliza desturi ya kukandiwa juu ya mfumo wake wa uchezaji 'kupaki basi' kwa kutumia soka ya kushambulia, ambayo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich anataka.
Kocha huyo Mreno, ambaye ameanza maandalizi ya msimu mpya wiki hii katika kipindi chake cha pili cha kufanya Chelsea, aliingia mzioni katika awamu yake ya kwanza akiwa na iPad.
Mourinho alitaniana na Frank Lampard na Gary Cahill wakati akikinoa kikosi chake kipya huko Cobham mchana. 
 Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Inter Milan mtindo wake uchezaji wa kujihami zaidi ulizaa maswali mengi siku za nyuma, lakini sasa anataka kuimarisha timu na kuwavutia mashabiki kwa soka ya kushambulia.
 "Nataka kuwafanya mashabiki wa Chelsea wafurahi – kwa matokeo, kwa mtindo wetu wa uchezaji, kwa uwezo wetu na haiba nzuri ya timu,"amesema.
"Wanatakiwa kujua kwamba, kuna matokeo ya aina tatu katika mechi – ambapo tunaweza kushinda, sare au kufungwa – lakini wakati wote tunajituma kwa kila kitu,". Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment