TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, July 8, 2013

BARCELONA YAMTENGEA PAUNI MILLION 30 DAVID LUIZ
david 65782
David Luiz ni mmoja kati ya mabeki bora
KLABU ya Barcelona imetangaza ofa ya Pauni Milioni 30 kwa ajili ya beki David Luiz – lakini Chelsea itagoma kumuuza kwa bei hiyo. (HM)
 Barca, ambao pamoja na ubora wao wote, wana hasara katika safu ya ulinzi, wanatarajiwa kuboresha ofa hiyo kwa ajili ya beki huyo mwenye kipaji ambao wanataka awe mbadala wa Nahodha wao, Carles Puyol.

Vyanzo vimesema ni 50/50 kwaLuiz kubaki Chelsea, ambako amekuwa mchezaji tegemeo tangu awasili Januari mwaka 2011 akitokea Benfica, au kuhamia kwa timu hiyo kubwa Ulaya.
 
Pamoja na uwezekano wa kuungana na Gerard Pique au Puyol katika safu ya ujlinzi, Luiz pia atakwenda kufanya kazi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Brazil akina Dani Alves na Neymar katika mfumo ambao anauwezea na unampendezea.

Msimu uliopita Barca iliteseka kutokana na Puyol kuwa nje kwa sababu ya maumivu, hivyo ikawalazimisha viungo Javier Mascherano au Alex Song kuhamia kwenye uinzi, hivyo Luiz kwa uwezo mkubwa hivi sasa ni mtu sahihi kwao. Chanzo: Sportmail

No comments:

Post a Comment