MOURINHO AMTENGEA PAUNI MILLION 60 ROONEY
Mshambualiaji wa Man U, Wayne Rooney (katikati) (HM)
Kocha wa Man U, David Moyes hivi karibuni alisema Rooney hauzwi
KLABU ya Chelsea itampa Wayne Rooney
mshahara wa Pauni 240,000 kwa wiki katika Mkataba wa miaka mitano dili
ambalo litamfanya akunje Pauni Milioni 60, kama atalazimisha kuondoka
Manchester United.
Rooney ni chaguo la kwanza la Jose
Mourinho katika usajili wa sasa na bosi huyo wa Chelsea ameendelea kuwa
na matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo majira haya joto.
Pamoja na kwamba Rooney aliambiwa na
David Moyes wiki iliyopita kwamba hataruhusiwa kuondoka United, kuna
mambo ambayo hayajatatatuliwa.
Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili
katika Mkataba wake Old Trafford, hajaonyesha dalili za kugeuza mawazo
yake na Chelsea inataka kutumia nafasi hiyo.
Atawagharimu kama Pauni Milioni 30 kama United watakubali kumuuza, lakini hiyo haitakuwa ngumu kwa Chelsea.
Mourinho, ambaye alianza kuinoa timu
hiyo jana baada ya kurejea tena majira haya ya joto, anataka kumpa
Rooney mwanzo mzuri Stamford Bridge.
Mourinho pia anafuatilia nafasu ya
Luis Suarez Liverpool na amewataka washauri wake kuendelea kumfahamisha
juu ya nafasi yake. Arsenal pia inamfuatili mshambuliaji huyo wa
Uruguay, lakini inabaki kuelekeza nguvu zake zaidi kwa Gonzalo Higuain
kutoka Real Madrid.
Higuain amekubali kujiunga na The
Gunners katika dili ambalo litamfanya Muargentina huyo akunje mshahara
wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Lakini klabu hizo bado zinapingana kwa
kiasi cha Pauni Milioni Milioni 2 katika ada ya uhamisho wake— na Real
inataka Pauni Milioni 25. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment