MAREKANI KUTOA NDEGE ZA KIVITA MISRI
MAREKANI inaendelea
na mpango wake wa kutoa ndege za kivita kwa jeshi la Misri licha ya
msukosuko wa kisiasa unaokumba nchi hiyo. Hatua hii inajiri wakati
Marekani ikiendelea kutathmini matukio ya wiki jana ambapo jeshi
lilimuondoa madarakani Rais Mohammed Morsi.
Msaada wa kijeshi kwa Misri
ungesitishwa endapo Marekani ingelitaja matukio ya wiki jana kama
mapinduzi ya kijeshi. Kundi la Muslim Brotherhood linalomuunga mkono
Morsi linasisitiza arejeshwe madarakani. (HM)
Wafuasi wake wamekua wakiandamana
karibu na kambi kuu ya jeshi ambapo anaaminika kuuzuiliwa. Hapo
Jumatatu,wafuasi wa Brotherhood 51 waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi
wakati wanakabiliano.
Utawala wa mpito umesema kwamba Bw. Morsi anazuiliwa eneo salama na kwamba haki zake zinazingatiwa.Maafisa wa Marekani wamesema ndege mpya za kivita aina ya F-16 zitawasilishwa katika wiki chache zijazo.
Mpango wa kufadhili jeshi ulianza kutekelezwa mapema mwaka huu na jeshi inatarajia kupokea ndege 20 za kivita. Msemaji wa ikulu ya Rais amesema Marekani haitabadilisha mpango wa kufadhili jeshi la Misri, japo inaendelea kutathmini kuhusu matukio ya kisiasa. Msaada wa kijeshi nchini Misri ambao hutolewa na Marekani hufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka.
Hapo Jumanne, kibali cha kumkamata kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohamed Badie kilitolewa pamoja na wakuu wengine tisa wa kundi hilo. Viongiozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia mjini Cairo ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa na mamia kujeruhiwa. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment