BROTHERHOOD KUENDELEA NA MAANDAMANO
KUNDI
la Muslim Brotherhood limeapa kuendelea na maandamano ya amani kupinga
kuondolewa madarakani kwa Rais Mohammed Morsi na jeshi la nchi. Wafuasi
wa Mosri wamekua wakiandamana mjini Cairo karibu na kambi kuu ya jeshi
anakoaminika amezuiliwa.
Taarifa ya Brotherhood inajiri wakati
kumetolewa kibali kuwakamata viongozi wake wakuu. Hapo Jumatatu wiki hii
wafuasi wa kundi hilo zaidi ya 50 waliuawa katika makabiliano na jeshi.
(HM)
Huku haya yakiarifiwa Marekani
imetangaza kwamba itatoa ndege za kivita aina ya F-16 kwa jeshi la Misri
katika majuma yajayo. Utawala wa Rais Barack Obama inaendelea
kutafakari matukio yaliyotokea Misri wiki jana.
Ufadhili wa jeshi ungesitishwa mara moja endapo mwingilio huo wa jeshi ungelionekana kuwa mapinduzi. Hapo Jumatano maafisa wa Misri walitoa kibali cha kukamatwa viongozi wa Muslim Brotherhood akiwemo kiongozi mkuu Mohammed Badie.
Viongozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia ambapo wafuasi wao waliuawa pamoja na maafisa watatu wa usalama. Tayari ratiba ya uchaguzi mpya imetangazwa na Rais mpya anatarajiwa kuchaguliwa mwakani sawa na bunge.
Katiba itafanyiwa marekebisho na kupigiwa kura ya maoni kabla ya mwisho wa mwaka huu.Kundi la Brotherhood limepinga mpango mpya na kuapa halitashiriki mchakato wowote bila Mohammed Morsi kurejeshwa madarakani. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment