DOLA BILLION 1.1 KUJENGA UPYA NIGERIA
CHINA imekubali
kutoa mkopo wa dola bilioni 1.1 kwa Nigeria ili kufadhili ukarabati wa
miundo msingi.Mkataba huu umeafaikiwa wakati wa ziara ya Rais Goodluck
Jonathan mjini Beijing,ambapo alikutana na mwenyeji wake Xi Jinping.
Fedha hizi zitasaidia ujenzi wa
barabara, viwanja vya ndege na kujenga miji minne na njia mpya ya
reli.China inawekeza kwa kiwango kikubwa Barani Afrika ambapo pia imekua
ikipata raslimali za mafuta na madini. (HM)
Nigeria inaongoza kwa kuzalisha mafuta
Afrika lakini kwa miaka imekua na miundo msingi mibovu, huku mamilioni
ya raia wake wakiishi kwa umasikini. Bw. Xi amesema nchi mbili
zinashirikiana kwa minajili ya kuboresha maisha ya watu wake.
Rais Jonathan anaongoza ujumbe wa wawekezaji wa Nigeria huko China na ziara ya siku nne itasaidia kuleta mshikamano wa karibu wa kibiashara.
Kampuni za ujenzi za Ki-China zimeanza kujenga barabara nchini Nigeria, kwa kandarasi ya dola bilioni 1.7.China kwa upande wake inatarajia kupata mapipa laki mbili ya matufa ghafi kutoka Nigeria ifikapo mwaka 2015. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment