TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, July 7, 2013

MAANDAMANO YAENDELEA MISRI

egypt 1eb11
MAANDAMAANO ya makundi hasimu yalifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo na katika maeneo mengine kote nchini humo  Jumapili, pale wafuasi na wapinzani wa Rais aliyeng’olewa madarakani Mohammed Morsi walipomiminika mitaani kutetea misimamo yao ya kisiasa. (HM)
Wafuasi wa Rais wa Morsi waliendelea kufanya mgomo wao mbele ya msikiti wa Rouba Adawiya mjini Cairo  huku wito ukitolewa wa kufanywa maandamano zaidi kote mjini humo.
Nao wapinzani wa Morsi pia wakipanga kufanya maandaamano yao  katika Tahrir Square.
Na huku maandamano ya kuunga na kumpinga rais Morsi yakiendelea, kaimu rais wa Misri Adly Mansour, anaendelea kujadiliana na viongozi wa upinzani juu ya kuunda serikali mpya.
Taarifa za Jumamosi kwamba  kiongozi wa  upinzani Mohammed ElBaradei amechaguliwa kuongoza serikali kama waziri mkuu, zilikanushwa na msemaji wa rais Ahmed Al Muslimany.
Alisema majadiliano yameanza lakini jina la waziri mkuu mpya bado halijaafikiwa. Alisema  Mohammed el Baradei ana nafasi nzuri zaidi  kuchukuwa wadhifa huo lakini maamuzi  rasmi bado hayajatolewa kwa vile mazungumzo ya kisiasa bado yanaendelea.
Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood  na wale wa chama cha Salafi Nour party, wanapinga uteuzi wa  ElBaradei.
Viongozi wa  Muslim Brotherhood wanasisitiza hawatashiriki katika utaratibu wowote wa mpito hadi pale rais wa zamani Morsi atakaporejeshwa  madarakani. Nao wanamgambo walilipua bomba  kuu la mafuta huko kaskazini mwa Sinai Jumapili na kusababisha moto mkubwa.  
Bomba hilo  linalopeleka  mafuta  kwa nchi jirani ya Jordan, limeshambuliwa mara kadha  tangu kupinduliwa kwa rais Hosni Mubarak hapo February mwaka 2011.Chanzo: voaswahili

No comments:

Post a Comment