MAHAKAMA nchini
Jordan imeshitaki Muhubiri wa Kiislamu Abu Qatada kwa makosa
yanayohusiana na Ugaidi baada ya kurejeshwa nchini Humo akitokea
Uingereza mapema hii leo.
Mashitaka ya kesi hiyo yamefuata yale ya mwaka 1999 dhidi yake.
Amesalia kwenye kizuizi chini ya gereza lenye ulinzi mkali kwenye eneo la jangwa nje kidogo ya mji mkuu wa Amman. (HM)
Kufika
kwa Abu Qatada nchini Jordan kumemaliza mabishano ya kisheria ya miaka
nane ya serikali ya Uingereza kutaka kumrejesha nchini Jordan,
Mabishano ambayo yameigharimu serikali ya Uingereza kiasi cha pound milioni mbili na nusu fedha za walipa kodi.
Mwandishi wa BBC mjini Amman amesema licha ya ahadi ya serikali ya Jordan ya kuendesha kesi hiyo kwa uwazi na usawa, lakini wanahabari wamezuiliwa kuingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo. Canzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment