Kiungo wa Vitesse Arnhem,Marco van Ginkel (HM)
KIUNGO wa Vitesse Arnhem, Marco van
Ginkel anajiandaa kukamilisha uhamisho wa kutua Chelsea, baada ya klabu
hizo kukubaliana biashara ya Pauni Milioni 9.
Van Ginkel, mwenye umri wa miaka 20,
ambaye amiechezea mechi moja Uholanzi, sasa anatakiwa tu kufuzu vipimo
vya afya na kukubali maslahi binafsi aliyopangiwa ili kuwa mchezaji wa
pili kusainiwa na Jose Mourinho baada ya Andre Schurrle.
Taarifa katika tovuti ya Chelsea
imesomeka: "Chelsea FC na Vitesse Arnhem zimefikia makubaliano ya
uhamisho wa Marco van Ginkel.
"Mchezaji huyo atajiunga na Chelsea
baada ya kufuzu vipimo vya afya, makubalino ya maslahi yake binafsi na
masuala ya kisheria,".
Van Ginkel alijiunga Vitesse akiwa na
umri wa miaka saba mwaka 1999 na kuendelea kukuzwa katika programu ya
vijana, kabla ya kuanza kukomazwa timu ya wakubwa mwaka 2010.
Amechezea vikosi vya vijana vya
Uholanzi chini ya miaka 19 na 21 na aliichezea kwa mara ya kwanza timu
ya wakubwa ya nchi hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani
mwaka jana.
Uhamisho huo utamfanya Mourinho awe
ametumia jumla ya kiasi cha Pauni Milioni 27 hadi sasa tangu amerejea
kupiga kazi Stamford Bridge kwa mara ya pili, baada ya awali kumsajili
mshambuliaji wa Kijerumani, Schurrle kutoka Bayer Leverkusen kwa mkataba
wa miaka mitano. Chanzo: Sportmail
No comments:
Post a Comment