TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, July 15, 2013

ARSENAL YAONGEZA DAU ILI KUMSAJILI SUAREZ
suarez2 b9c8b
KLABU ya Arsenal imeendeleza dhamira ya kumsajili Luis Suarez na wiki hii itapanda dau hadi Pauni Milioni 35 kwa ajili ya nyota huyo wa Liverpool anayetaka kuondoka. (HM)
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uruguay kwa sasa ni chaguo namba moja la Arsene Wenger katika usajili wa majira haya ya joto na iko tayari kutoa dau kumhamishia Emirates Stadium.

Arsenal imeshuhudia ofa yao ya awali ikipigwa chini Merseysiders, ambayo inataka Pauni Milioni 40 angalau ili kumuuza nyota huyo wa Amerika Kusini.

Wakiwa wameona dau lao la Pauni Milioni 30 limepigwa chini, The Gunners itampandia dau mchezaji huyo wiki hii.
Matumaini yanakuwa kwa wapenzi wa Arsenal kwamba, dili hilo si masihara na klabu itatumia sehemu ya Pauni Milioni 70 ilizotenga kwa ajili ya usajili kumnasa Suarez.
Wenger anakabiliwa na changamoto ya kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia majira haya ya joto baada ya taarifa tofauti kusema kwamba klabu ipo katika nafasi nzuri kifedha kusaini kipoaji cha hali ya juu.

Dau la Pauni Milioni 23 kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain, ambaye atarejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Real Madrid leo, kimsingi limekubaliwa. Chanzo: Binzubeiry

No comments:

Post a Comment