TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, July 15, 2013

MAN UNITED YAWEKA MEZANI CAM NOU PAONI 26 MIL KUMNASA FABREGAS
fab d3a9d
KLABU ya Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kutaka kumsajili Cesc Fabregas baada ya Mashetani hao Wekundu kuweka mezani Pauni Milioni 26 kwa ajili ya kiungo huyo wa Barcelona. (HM)
Timu ya David Moyes imekuwa ikihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye amekuwa akipambana kuwa mchezaji muhimu kwa mabingwa hao wa Hispania.
Lakini baada ya kumkosa mchezaji mwenzake wa Barca, Thiago Alcantara kufuatia nyota huyo wa timu ya taifa ya Hispania chini ya umri wa miaka 21 kuamua kujiunga na Bayern Munich, tmabingwa hao wa Ligi Kuu England sasa wako tayari kutumia fedha zaidi kuhakikisha mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania anarejea England.
Klabu ya zamani ya Fabregas, Arsenal inaweza kupiga bao katika dili ikitaka, kutokana na The Gunners kupewa kipaumbele cha kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward hivi karibuni amesema kwamba klabu iko tayari kushindana kugombea wachezaji hata kwa dau la Pauni Milioni 60 hadi 70 na kwamba wanataka kusajili wachezaji wakubwa duniani.

Klabu ya zamani ya Fabregas, Arsenal inaweza kupiga bao katika dili ikitaka, kutokana na The Gunners kupewa kipaumbele cha kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward hivi karibuni amesema kwamba klabu iko tayari kushindana kugombea wachezaji hata kwa dau la Pauni Milioni 60 hadi 70 na kwamba wanataka kusajili wachezaji wakubwa duniani. Chanzo: Binzubeiry

No comments:

Post a Comment