BINTI KIZIWI ATUPWA JELA MIAKA MITANO BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA
MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu.
Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo,mwandishi wetu alilazimika kuwatafuta ndugu zake ili kuujua ukweli
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu yake, Binti kiziwi hajanyongwa bali ametupwa jela miaka mitano.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
DEMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo.
No comments:
Post a Comment