TAIFA STARS YA KIM PAULSEN KUANZA COSAFA JULAI 6
Taifa Stars imepangwa kundi A la
michuano ya Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6
mwaka huu jijini Lusaka, Zambia dhidi ya Shelisheli.
Upangaji ratiba (draw) wa mashindano
hayo ulifanyika Mei 3 mwaka huu jijini Lusaka ambapo timu nyingine
zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo ni Namibia na Mauritius. Kundi
la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka.
Mechi ya pili ya Taifa Stars katika
hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya
mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia.
Kundi B lina timu za Kenya (Harambee
Stars), Botswana (Zebras), Lesotho na Swaziland. Hatua itakayofuata
baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa timu moja
tu.
Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai
13 mwaka huu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu
nyingine tano zimekwenda moja kwa moja katika hatua ya mtoano.
Nyingine zilizokwenda moja kwa moja
hatua ya mtoano ni wenyeji Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi
ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment