RAIS WA TFF KUZINDUA KOZI YA MAKOCHA JUMATATU DAR ES SALAAM
RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi ya makocha wa ngazi
ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumatatu (Juni 3, 2013) kwenye
Ukumbi wa Hobours Club, uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph
Kanakamfumu, alisema Rais Tenga atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
kozi hiyo itakayohusisha amakocha 26.
Alisema
kozi hiyo itakayomalizika Juni 28 itakuwa imewezesha kupatikana makocha
watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na
Taifa kwa ujumla.
Aliwataja
makocha wa kozi hiyo kuwa ni Shadrack Nsajigwa, Benard Mwalala, Steven
Nyenge, Jemedari Said Kazumari, Zubeiri Katwila, Ibrahim Masoud
‘Maestro’, David William Ngaga, Idd Abushir Mwinchumu, Rajab Mohamed
Nakuchema, Lubigisa Madata, Bakari Mahad, Greyson Swai, Chiwanga A.
Chiwanga, Sizza Mapunda na Muhibu Kanu.
Wengine
ni Omari Mbarouk, Omari Mohamed, Samuel Galafawo, Abdallah Mbogolo,
Hassan Msonzo, Akida Said, Emanuel Gabriel, Barton Msengi, Edgar Method
Katembo, Elly Kaiza na Renatus Benard.
Kozi
hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia kwa uongozi mpya wa
chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas Kassongo.
Wengine
walioingia madarakani katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa
Hoteli ya Mbezi Garden ni Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu
Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny
Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.
No comments:
Post a Comment